NA MWAJUMA JUMA

UONGOZI wa kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM) umejiandaa kusajili wachezaji wenye uwezo wa kukabiliana na mashindano ya kimataifa.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa kikosi hicho, Komodoo Azana Hassan Msingiri, alipozungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Kibweni.

KMKM inatarajiwa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kuwa bingwa wa Zanzibar, katika ligi kuu ya Zanzibar iliyomalizika hivi karibuni.

Msingiri alisema kwa sasa wameingia mkataba na mfadhili wa Simba Mohamed Dewji ‘Mo’, ambae aliwahakikishia kushirikiana nao katika mambo mbali mbali, ikiwemo kuwaletea makocha ambao watawapa mbinu za ushindani wa mashindano hayo.

“Mo tumekubaliana atusaidie mambo madogo madogo na nina amini timu yetu itashiriki vyema michuano hiyo”, alisema.

Alifahamisha kwamba kusajili wachezaji wenye viwango vya kimataifa na wenye sifa kulingana na mashindano yenyewe.

“Kwa mwaka huu sisi ndio tutakuwa wa kwanza kusajili wachezaji wenye ubora, tutaingia gharama yoyote bila ya kujali isipokuwa tutafanya hivyo ili kuona tunaiwakilisha vyema nchi yetu”, alisema.