NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya soka ya KMKM imeondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mafunzo katika mechi ya kirafiki.Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Mao Zedong majira ya saa 3:00 asubuhu.

Hadi timu hizo zinakwenda  mapuziko KMKM ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili,huku Mafunzo ilikuwa haijapata kitu.

Mabao hayo yaliwekwa wavuni na Mussa Ali Mbarouk dakika ya 23 na bao la pili liliomgezwa na Is-haka Said dakika ya 34.

Kurudi uwanjani   kumalizia kipindi cha pili timu hizo ziliingia na kasi kubwa kila mmoja kutaka nafasi ya kuingiza bao kwenye mlango wa mwenzake.

Dakika ya 58 Abrahman Othman wa KMKM aliongeza bao la tatu na bao la kufutia machozi la Mafunzo liliingizwa na Rashid Ali dakika ya 88.