KABUL, AFGHANISTAN

RAIS wa Afghanistan Ashraf Ghani, kuachiliwa huru wafungwa 5,000 ambao walikuwa wanachama wa kundi la wanamgambo wa Taliban ni miongoni mwa makosa makubwa kuwahi kufanyika.

Akizungumza baada ya sala ya Eidul-Adh’ha, rais Ghani alikosoa hatua ya kundi la Taliban ya kuendesha mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kueleza kwamba, wanamgambo hao hawataki kuona amani na usalama vinarejea nchini humo.

Rais Ghani alisema Taliban hawana nia ya dhati kuiona nchi hiyo ina amani ya kudumu na kwamba kuachiliwa huru maelfu ya wanachama wake waliokuwa wakishikiliwa jela hakujalifanya lishiriki mazungumzo ya amani na serikali ya Kabul.

Rais huyo alisema hayo katika hali ambayo, duru nyingine ya mazungumzo ya wawakilishi wa serikali na wanamgambo wa Taliban inaendelea huko mji Doha nchini Qatar.

Alisema serikali yake imetuma ujumbe wa ngazi za juu katika mazungumzo hayo huko Qatar ili kutimiza hoja na kuwathibitisha walimwengu kwamba, ni jinsi gani inavyolipa umuhimu suala la mazungumzo ya kutafuta amani.

Katika hatua nyengine rais Ghani alisema ameikosoa serikali ya Pakistan kwa kueleza kuwa nchi hiyo ina inalisaidia kwa siri kundi hilo la wanamgambo wanaoendesha vitendo vya kigaidi.