NA MWANAHAWA HARUNA SCCM
TIMU ya soka ya KVZ chini ya umri wa miaka 21 imewalalamikia baadhi ya waamuzi wa michuano ya Vumbua inayoendelea kuchezwa katika hatua ya robo finali.
Akizungumza na gazeti hili uwanja Mnazi Mmoja katibu wa timu hiyo Khamis Abdalhamud Hamidi,
“Changamoto katika michezo ni jambo la kawaida lakini waamuzi nahisi wanashidwa kufanya majukumu yao, kwa kufanya maamuzi yasio sahihi, sio kwamba hawajui lakini hawafuati sheria ,” alisema.
Pia amewataka waandaji wa michuano hiyo kuangalia tena suala la waamuzi hususani katika hatua inayo endelea ya robo fainali na hatua nyengine.
Naye nahodha wa timu hiyo Rashid Hamid Shindano amelezea kuwa katika michuano hiyo, wanakumbana na changamoto ya kucheza katika viwanja ambavyo havina ubora kitu ambacho kinapelekea kupoteza baadhi ya mechi.
Pia amewatoa hofu mashabiki wa KVZ kuwa watarajie mazuri katika michuano hiyo na kupata ushidi.