WIZARA ya ulinzi ya Marekani Pentagon, inatekeleza agizo la rais wa nchi hiyo Joe Biden la kuwaondosha wanajeshi wake nchini Afghanistan ambao walikuwemo nchini humo kwa takriban miaka 20 wakipambana na kile kilichoitwa mizizi ya ugaidi.

Kwa muhibu wa taarifa hadi kufikia Gosti 31 mwaka huu Marekani itakuwa imeondisha wanajeshi wake wote na watabakia wachache sana kwa ajili ya kulinda maeneo muhimu zikiwemo balozi za nchi hiyo.

Marekani baada ya kuwaondosha wanajeshi wake nchini humo umepnga   kuendelea kutoa msaada wa kifedha na vifaa kwa wanajeshi wa Afghanistan ili kupambana na kundi la Taliban.

“Lengo letu kuu sasa katika kwenda mbele ni kuhakikisha kuwa, machafuko, ugaidi haviwezi kuhamishwa kutoka Afghanistan hadi kwenye nchi yetu”, alisema waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin.

Kwa wakati huu wanajeshi wengi wa Marekani na kutoka nchi washirika wakiwa wameshaondoka nchini humo kundi la Taliban ambalo limepambana na kwenye vita kwa muda miaka 20 sasa limejiimarisha upya.

Mkuu wa baraza la kijeshi Marekani Jenerali Mark Milley amesema kundi la Taliban linaonekana kuwa na muendelezo wa kimkakati katika mapambano na linataka kuidhibiti wa Afghanistan, huku miji kadhaa ikiwa mikononi mwao.

Jenerali Miley alisema wataliban wanadhibiti zaidi ya nusu ya wilaya 419, lakini bado hawajakamata mji mkuu wowote kati ya mikoa 34 ya nchi hiyo hata hivyo wameongeza shinikizo kwa karibu nusu ya miji hiyo.

Kwa wakati huu kuna wasiwasi mkubwa nchini Afghanistan kutokana na wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo kuelelewa na wapiganaji wa Taliban katika maeneo mbalimbali.

Katika hatua ya kushangaza sana huku wananchi wa Afghanistan wakiwa hawajui hatma yao, raia katika nchi jirani ya Pakistan wanawaunga mkono wapiganaji wa Taliban.

Hali hiyo imeashiria ushawishi wa kundi hilo miongoni mwa raia wa Pakistan na Afghanistan. Siku za hivi karibuni nchi hizo mbili zilitupiana lawama kuhusu swala la kuwaunga mkono wapiganaji wa Taliban.

Mfano mmoja wapo ni kijana Abdul Rasheed raia wa Pakistan aliyefariki kwenye jimbo la Ngangarhar nchini Afghanistan mapema mwezi huu. Mamia ya watu waliohudhuria mazishi ya kijana huyo wa miaka 22 karibu na Peshawar walisikika wakiimba nyimbo zinazounga mkono kundi la Taliban.

Kwenye mitandao ya kijamii, picha za video za raia wa Pakistan waliobeba bendera za Taliban na kuimba nyimbo za kundi hilo zilizagaa mitandaoni. Hayo yametokea wakati ambapo wapiganaji wa Taliban wanaendelea kuyadhibiti maeneo kadhaa ya Afghanistan huku vikosi vya mwisho vya Marekani na washirika wake vikiwa vinakaribia mwisho wa uwepo wake nchini humo.

Wahubiri wa kiislamu kwenye maeneo kadhaa ya Pakistan wamekuwa wakiwahimiza raia kuwaunga mkono Wataliban na kutoa wito wa kupatiwa misaada ili wafanikiwe kuidhibiti nchi hiyo.

Wakaazi wengi kwenye mji wa Quetta na mkoa wa Pishin, jimboni Balochistan, wamekaririwa wakisema kuwa kuna ongezeko la watu wa Pakistan wanaowaunga mkono Wataliban.

Hata hivyo mkaazi mmoja alisema japo kuwa Wataliban wanaungwa mkono kwenye eneo lao, maandamano ya kuwapinga hayawezi kufanikiwa bila kuungwa mkono wa viongozi wa serikali.

Alisema mwanzoni wahubiri walikuwa wakiomba michango misikitini kwa ajili ya Taliban, lakini hivi sasa wanapita nyumba hadi nyumba kuomba michango ambayo ni kwa ajili yakuwasaidia wapiganaji wa vita vitakatifu vya Afghanistan.

Lakini maofisa wa Pakistan wamesema taarifa hizo za maandamano ya kuwaunga mkono na misaada kwa Wataliban ni za uzushi. Zahid Hafeez Chaudhary, msemaji wa wiraza ya mambo ya nje ya Pakistan alisema kuwa madai hayo hayana msingi wowote na hayatokei nchini humo.

Kundi la Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP) limepigwa marufuku nchini Pakistan, lakini wataalamu wanasema tuhuma za kwamba serikali inaliunga mkono unalipa nguvu kundi hilo.

Wanamgambo wa Taliban wameyadhiti maeneo kadhaa nchini Afghanistan katika siku za hivi karibuni na wamekuwa wakiwahimiza raia wa Pakistan kujiunga nao nchini Afghanistan.

Hivi karibuni watu kadhaa kutoka nchini Pakistan waliuliwa kwenye uwanja wa mapambano kutokana kuwaunga mkono Wataliban dhidi ya vikosi vya serikali.

Wachambuzi wamesema viongozi wa Pakistan hawajachukuwa hatua yeyote kuzuia raia wake kujiunga na Wataliban kwenye nchi jirani ya Afghanistan.

Mitandao ya kijaami imekuwa ikionyeshaa picha za mazishi ya wapiganaji waliouliwa nchini Afhganistan ambapo mamia ya watu walihudhuria mazishi ya wapiganaji wa Pakistan ambao miili yao ilirejeshwa makwao.

Michael Kugelman, naibu mkuu wa taasisi ya Wilson Center kuhusu Asia kusini amesema uungwaji mkono wa Pakistan sio tu kuigeuza ardhi yake kuwa maficho kwa viongozi wa kundi la Taliban bali pia huduma za kiafya kwa kundi hilo na kwa familia za wapiganaji wake.

Kugelman alisema msimamo wa Pakistan wa hapo awali wa kupatanisha kundi la Taliban na Marekani na baadae taliban na serikali ya Afghanistan, umetofautiana na madai kwamba haina ushawishi wa kutosha dhidi ya Wataliban.

Alisema kunauungwaji mkono mkubwa wa Wataliban nchini Pakistan na kwa miaka kadhaa raia wa Pakistan wamejiunga na kundi la taliban akama wapiganaji.

Vita vya maneno viliongezeka mwezi huu kati ya Afghanistan na Pakistan baada ya Makamu wa Rais wa Afghanistan kulituhumu jeshi la Pakistan kwa kutoa msaada wa angani kwa Taliban katika maeneo fulani, hata hivyo Pakistan imekanusha vikali madai hayo.