NA MWAJUMA JUMA

LIGI Kuu ya Zanzibar ya mpira wa Kikapu Kanda ya Unguja kwa wanaume na wanawake itaendelea Julai 29.

Ligi hizo ambazo ilisimama kupisha misiba ya viongozi wa kitaifa na mashindano mengine yaliyoandaliwa na chama cha mpira huo Zanzibar (BAZA),  inazishirikisha timu 12 zikiwemo nane za wanaume nne za wanawake.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo iliyotolewa na kamati ya mashindano ya chama hicho ligi hizo zitakuwa zikichezwa katika viwanja vya Mao Zedong na Maisara.

Timu zinazoshiriki ligi hiyo kwa wanaume ni African Magic, JKU, Millenium, New West, Nyuki, Polisi, Stone Town na Usolo za wanawake JKU, KVZ, KZU na New West.

Ratiba ya ligi hiyo ya wanaume inaonesha kwamba kwa siku kutakuwa kukichezwa mechi mbili, ambapo katika uwanja wa Mao Zedong na Maisara.

Ligi  B inashirikisha timu saba ambazo ni Beit Raas, Cavarious, Good Morning, KZU, Mbuyuni na Sixers nazo michezo yote itakuwa ikichezwa katika viwanja vya Maisara na Mao Zedong.