LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Jesse Lingard anawindwa na timu ya Atletico Madrid, na kuna uwezekano mkubwa timu hiyo ikamuuza.

Kinda huyo alifanikiwa kuonyesha kiwango cha juu akiwa na West Ham msimu uliopita, na aliaminika kuwa anaweza kubaki kwenye timu hiyo lakini United wamegoma.

Wamepeleka ofa ya kumtaka mchezaji huyo mwenye uwezo wa juu wa kufunga mabao, wakiwa wanaamini kuwa anaweza kuwasaidia msimu ujao.

Timu hiyo chini ya kocha Diego Simeone imepeleka ofa mara mbili kwa ajili ya mchezaji huyo, ambaye pia amepelekewa ofa ya West Ham.

United wanataka kitita cha pauni milioni 15 kwa ajili ya mchezaji huyo, lakini tayari Atletico wamepeleka ofa ya milioni 10, huku West Ham wakiishia milioni 8.