LONDON, England
KLABU ya Liverpool wamemuuza kiungo, Marko Grujic kwa Porto kwa pauni milioni 10.5 na mshambuliaji, Taiwo Awoniyi kwenda Union Berlin kwa pauni milioni 6.5.

Nyota wa kimataifa wa Serbia, Grujic (25), alitumia msimu uliopita kwa mkopo huko Porto, akicheza mechi 28 za ligi na mechi nane za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mnigeria Awoniyi (23), alifunga magoli matano katika michezo 22 akicheza kwa mkopo huko Union Berlin ya Ujerumani msimu uliopita.

Liverpool wamejadili asilimia 10% ya vifungu vya kuuza katika mikataba yote miwili.
Grujic alikua usajili wa kwanza wa meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp wakati akijiunga

akitokea Red Star Belgrade mnamo Januari 2016 kwa pauni milioni 5.1.
Alicheza mechi 16 za Liverpool, wakati pia alitumika kwa mkopo huko Cardiff City, Hertha Berlin na Porto.

Awoniyi, aliyejiunga na Liverpool mnamo Agosti 2015, hakuonekana kwenye klabu hiyo na alipewa tu kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza mnamo Mei.
Amekuwa kwa mkopo huko FSV Frankfurt, NEC Nijmegen, Royal Excel Mouscron, Gent, Mainz na Union Berlin wakati akiwa na Liverpool.(BBC Sports).