LONDON, Engalnd

MANCHESTER City wapo kwenye mpango wa kuipata saini ya beki kisiki Sergio Ramos kwa dili la miaka miwili kwa mujibu wa ripoti.

Beki huyo raia wa Hispania ikiwa dili lake litajibu atajiunga na timu hiyo bure kwa kuwa mabosi wake wa zamani Real Madrid hawajamuongezea mkataba mpya baada ya dili lake kumeguka rasmi Juni 30.

Licha ya kwamba City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola ikiwa inahitaji kupata saini yake ripoti zinaeleza kwamba Barcelona nao wanahitaji huduma yake sawa na PSG, ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kupata saini ya beki huyo ambaye amecheza kwa muda wa miaka 16 ndani ya Real Madrid na alikuwa nahodha pia.

Imani kubwa ya kocha Guardiola kwa Ramos ni kwenye suala la uongozi hivyo anaamini kwamba akipata saini yake itamuongezea nguvu kwenye ushindani ndani ya Ligi Kuu England.