KWA mujibu wa taasisi ya utafiti wa amani mjini yenye makao yake mjini Stockholm nchini Sweden (SIPRI), imebainisha kuwa gharama ya ununuzi wa silaha duniani imepanda hadi kufikia dola bilioni 1981 kufikia mwaka 2020.

Ongezeko hilo la matumizi ya fedha za silaha ni sawa na asilimia 2.9 ikilinganishwa na matumizi kama hayo kwa mwaka 2019, kwa mujibu wa utafiti wa taasisi hiyo.

Katika mwaka 2020 yapo mataifa yaliyotumia fedha nyingi zaidi ambapo data zinaonesha kuwa yalitumia asilimia 62 ya fedha zote zilizotumika kununua silaha duniani ni pamoja na Marekani, China India Urusi, India na Urusi.

Kwa mujibu wa SIPRI, matumizi ya ununuzi wa silaha uliofanywa na China lililoko mashariki ya mbali yaliyongezeka kwa mara 26.

Mnamo mwaka 2017 Marekani ilitumia asilimia 3.1 ya mapato yake kununua silaha ikiwa ni robo ya matumizi ya taifa lililotumia fedha nyingi zaidi kununua silaha.

Pamoja na hali hiyo ni wazi kwamba Marekani haipo katika mataifa 20 ambayo hutumia utajiri wao kununua silaha za kijeshi, makala haya yanakuletea nchi 10 ambazo zinaongoza katika orodha ya ununuzi wa silaha.

Bahrain: Taifa hilo linalotawaliwa na ufalme wa madhehebu ya sunni linashilinia nafasi ya 10 katika orodha hiyo, lakini wengi wa raia wake ni wislamu wa madhehebu ya shia, suala ambalo limekuwa likizua hali ya wasiwasi katika taifa hilo.

Mnamo mwaka 2011, wakati wa mapinduzi ya Arabuni au Arab Uprising, wanajeshi wa baraza la Ghuba walipelekwa katika taifa hilo kuzuia maandamano.

Katika mwaka 2017 taifa hilo lilitenga dola milioni 1,396m katika matumizi yake kwenye sekta ya ulinzi ikiwa ni asilimia 4.1 ya mapato yake kulingana na makadirio ya Sipri.

Urusi: Mnamo mwaka mwaka 2017, Urusi kwa mara ya kwanza ilipunguza matumizi yake ya ununuzi wa vifaa vya kijeshi tangu 1998 ikishusha matumizi yake kwa asilimia 20 na kufikia dola milioni 66,335 ikiwa ni sawa na asilimia 4.3 ya pato lake la nchi.

Kulingana na Siemon Wezeman, mchunguzi mkuu katika taasisi ya SIPRI, punguzo hilo linatokana na matatizo ya kiuchumi ambayo taifa hilo limekuwa likishuhudia tangu 2014, kwasababu kuliimarisha jeshi lake kufikia viwango vya kisasa kumekuwa kipao mbele cha Moscow.

Lebanon: Taifa hilo liliopo mashariki ya kati ni kati ya mataifa kumi yalio na mzigo wa kijeshi duniani, mataifa sita yanatoka eneo la mashariki ya kati. Na taifa la Lebanon ni miongoni mwao.

Taifa hilo lilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1975 na 1990 na tangu wakati huo maisha yake ya kisiasa yamekumbwa na mgawanyiko mkubwa.

Sera yake ya nyumbani na ile ya kigeni imeshawishiwa na majirani zake Syria, pamoja na nguvu ya kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Hezbollah ambalo mwaka 2006 lilipigana vita dhidi ya Israel. Matumizi yake ya kijeshi yalifikia dola milioni 2,441 sawa na asilimia, 4.5% ya pato lake.

Israel: Tangu lilipoanzishwa 1948, taifa la Israel limezungukwa na maataifa inayodai kuwa maadui zake. Hali hiyo ilirekebishwa baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani na Misri 1979 na Jordan 1994.

Hata hivyo taifa hilo bado linaendelea kuwa na maadui hususan katika mpaka wake na Syria pamoja na wapiganaji wa Lebanon wa Hezbollah ambao ni washirika wa Iran, moja wapo ya mataifa ambayo hayaonani macho kwa macho na Israel.

Kulingana na Sipri, jeshi la Israel kufikia mwaka 2017 lilikuwa likitumia dola milioni 16,489 ambazo ni aslimia 4.7%ya pato lake.

Jordan: Ni taifa lilijipatia uhuru mwaka 1946 na tangu wakati huo limekumbwa na hali ya wasiwasi kutokana na mazingira ya mzozo.

Mwaka 1967, wakati wa vita vya siku sita dhidi ya Israel, taifa hilo lilipoteza eneo la West Bank na Jerusalem maeneo ambayo ilikuwa ikiyamiliki tangu vita vya Waarabu na Israel 1948.

Mwaka 1984, alitia saini makubaliano ya amani na Israel hatua ambayo haimkingi na tatizo la usalama linaloendelea kukumba eneo hilo, kama lile linalosababishwa na Islamic State.

Mwaka 2017, lilitenga dola milioni 1,939 katika sekta ya ulinzi ikiwa ni sawa asilimia 4.8% ya pato lake la nchi.

Algeria: Ni taifa linalokubwa vipindi vikali vya ghasia katika historia yake kama taifa huru ambavyo vilianza 1962. Baadhi ya vipindi hivi vimetokana na hali ya wasiwasi kati ya makundi ya kidini na yale ya kidunia ya jamii yake.

Kati ya 1992 na1998, taifa hilo lilikumbwa na mzozo wa ndani kwa ndani ambao ulisababisha zaidi ya vifo 100,000 baada ya kufutwa uchaguzi ambapo kundi la Islamic Salvation lilionekana kana kwamba litaibuka mshindi.

Tangu wakati huo, taifa hilo limeendelea kuathiriwa na ghasi, lakini pia limekumbwa na mashambulio kutoka kwa makundi ya wapiganaji kama vile lile la Al Qaeda kutoka Islamic Maghreb.

Mwaka 2017, liliandikisha matumizi ya yanayokadiriwa na Sipri kuwa dola milioni 10,073 ikiwa ni sawa na 5.7% ya pato lake la taifa.

Kuwait: Likiwa na ardhi yenye ukubwa wa kilomita 17,818 na watu milioni nne, Kuwait ni taifa dogo lililozungukwa na majirani wakiwemo Saudi Arabia, Iran na Iraq.

Taifa hilo linamiliki kambi kadhaa za Marekani ambapo baadhi ya majeshi ya muungano wa kimataifa unaopigana dhidi makundi ya kundi la Islamic State yanaishi. Mwaka 2017, lilitenga matumizi ya dola milioni 6,831, sawa na asilimia 5.8% ya pato lake.

Congo: Likitumia asilimia 6.2 ya pato lake katika vifaa vya kijeshi, Jamhuri ya Congo ndio taifa la Afrika linalotenga utajiri wake mkubwa katika sekta ya ulinzi likitenga dola milioni 484 kulingana na makadirio ya Sipri.

Taifa hilo limeshuhudia vipindi kadhaa vya mizozo ya ndani kwa ndani chini ya uongozi wa Denis Sassou-Nguesso, mwanajeshi wa zamani ambaye alitawala taifa hilo kati 1979 na 1992 na ambaye alirudi madarakani 1997 na ambaye amesalia hadi sasa.

Saudi Arabia:  Tangu 2015, serikali ya Saudia Arabia imeongoza kundi la mataifa katika vita vya Yemen dhidi ya waasi wa Houthi ambao wanaungwa mkono na Iran.

Tukio hilo ni mojawapo ya baadhi ambapo Riyadh na Tehran zinapigania udhibiti wa kisiasa, na kiuchumi wa eneo zima la mashariki ya kati.

Ufalme wa Saudia pia hushiriki katika muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State. Kulingana na Sipri taifa hilo lilitenga dola milioni 69,413 sawa na asilimia 10 ya pato lake.

Oman: Ndio taifa nambari moja duniani lenye kutumia utajiri wake katika ununuzi wa silaha. Oman ikiwa katika eneo la kimkakati la mkondo wa Hormuz, mojawapo ya maeneo muhimu ambayo meli za mafuta hupita na likiwa na majirani kama vile Iran, Saudi Arabia na Yemen.

Ufalme wa Oman umeongeza matumizi yake ya kijeshi katika kipindi cha miongo kadhaa iliopita, ambapo katika mwaka 2017, taifa hilo lilitenga dola milioni 8,686 sawa na asilimia 12% ya pato lake kwa ajili ya ununuzi wa silaha.