NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya soka ya Mboriborini imeanza vyema kampeni yake kutetea taji la Yamle Yamle cup baada ya kuifunga Black Lion bao 1-0.

Mboriborini ambayo ilishuka dimbani juzi ikiwa ni mchezo wake wa awali uliochezwa uwanja wa Magirisi.

Katika mchezo huo miamba hiyo yote kwa pamoja ilicheza mchezo wa kukamiana ambao ulitoa burudani tosha kwa umati wa mashabiki waliohudhuria uwanjani hapo.

Wakicheza kwa kila mmoja kukumbuka tambo zake wanaume hao walikwenda mapumziko wakiwa hawakufungana.

Kuanza kwa kipindi cha pili kila mmoja alionekana kuwa na ari na nguvu mpya na kufuata maelekezo mazuri kutoka kwa walimu wao.

Ilikuwa zimebakia dakika tatu kumalizika kwa mchezo huo ndipo Saleh Masoud Tumbo akaifungia timu yake hiyo bao ambalo liliwafanya waondoke na pointi tatu.

Itakumbukwa kwamba mchezaji huyo ambae aliifungia timu yake bao hilo la pekee ndie huyo huyo ambae aliifungia timu yake bao katika mchezo wa ngao ya hisani na kuibuka na ubingwa wa ngao hiyo na kujichukulia shilingi milioni moja.

Leo michuano hiyo itaendelea tena kwa kuchezwa michezo miwili ambapo katika uwanja wa Magirisi Meli nne city itacheza na Haturudi nyuma na JKU Academy na Mtende City watacheza katika uwanja wa Amani nje,  michezo ambayo itachezwa majira ya saa 10:00 za jioni.