PARIS, UFARANSA

UFARANSA imesema kuwa mamlaka za usalama nchini Morocco zilijaribu kudukua simu ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kutumia waya wa udukuzi uliotengenezwa nchini Israeli -Pegasus spyware.

Makundi ya kutetea haki za binadamu Forbidden Stories na Amnesty International yanasema kuwa Morocco ilitambua simu ambayo rais Macron amekuwa akiitumia tangu mwaka 2017.

Haijafahamika wazi iwapo waya huo wa Pegasus uliwahi kutumiwa na Morocco katika kutekeleza jaribio la kudukua mawasiliano ya rais huyo.

Katika jaribio hilo, mawaziri kadhaa wa Ufaransa walidaiwa kufuatiliwa ma mamlaka za Morocco ili kujaribu kuwadukua akiwemo waziri mkuu wa zamani Edouard Philippe.

Namba zao za simu zilikuwa miongoni mwa namba 50,000 ambazo zilikuwa zimezoorodheshwa kati ya namba zinazoweza kudukuliwa.

Ripoti hiyo ilisema kuwa ufuatiliaji wa kidigitali wa nyaya za udukuzi wa pegasus ulikuwepo kwenye makumi ya nambari hizo za simu.

Watengenezaji wa pegasus, NSO Group, wanasema huuza kifaa hicho kwa serikali zilizochunguzwa kwa ajili kukabiliana na uhalifu na ugaidi.

Waendesha mashtaka jijini Paris, wameanza uchunguzi wa madai ya maofisa wa ujasusi wa Morocco, kutumia kampuni ya masuala ya ujasusi wa mtandao, Malware Pegasus kuwadukua wanahabari wa Ufaransa.