LONDON, England

JOSE MOURINHO amemtaja Luke Shaw kati ya wachezaji ambao walipaswa kujitokeza kupiga penalti kwa England, badala ya Bukayo Saka dhidi ya Italia kwenye fainali ya Euro 2020.

England ilifungwa kwa mikwaju ya adhabu penalti dhidi ya Italia huko Wembley Jumapili usiku na Marcus Rashford, Jadon Sancho na Saka walikosa.

Gareth Southgate aliwaingiza Rashford na Sancho kutoka benchi dakika za mwisho za muda wa nyongeza haswa kwa mikwaju ya penalti.

Baada ya Rashford kugonga mwamba na Sancho iliokolewa na Gianluigi Donnarumma, iliachwa kwa Saka mwenye umri wa miaka 19 kuweka matumaini ya England hai, huku kipa wa Italia akafuta matumaini ya kabisa ya England kutwaa taji hilo.

Nahodha wa zamani wa Manchester United Roy Keane alikuwa miongoni mwa wale waliohoji kwa nini wachezaji wakubwa zaidi Raheem Sterling na Jack Grealish hawakujitokeza kupiga penalti.

‘Katika hali hii, Raheem Sterling alikuwa wapi? John Stones alikuwa wapi? Luke Shaw alikuwa wapi? Kwa nini Jordan Henderson au Kyle Walker hawakubaki uwanjani’’ alihoji Mourinho