MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Isdor Mpango, amehudhuria ufunguzi wa Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa.

Makamu wa Rais anamwakilisha, Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa hilo lenye madhumuni ya kuchagiza Usawa wa kijinsia linajadili Umuhimu wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kama nyenzo ya kumnyanyua mwanamke kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Kati ya mambo yaliyojadiliwa katika jukwaa hilo ni kumwezesha mwanamke kupata Teknolojia rahisi na sahihi katika kufanya shughuli za kiuchumi; kutolewa mafunzo ya ujasiriamali.

Mambo mengine ni pamoja na utoaji wa mitaji kwa wanawake pamoja uwepo wa mifumo sahihi ya kidigitali katika shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanawake.

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, anatarajia kutoa Ahadi za Tanzania  kama kinara wa uwezeshaji wanawake kiuchumi  kama ilivyoridhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.