WASHINGTON, MAREKANI
MWENYEKITI wa kamati iliyosimamia kuapishwa kwa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump mwaka 2017, amekamatwa kwa madai ya kujaribu kushawishi sera za kigeni za Trump kuupendelea Umoja wa Falme za Kiarabu.
Thomas Joseph Barrack wa Santa Monica, California, mwenye umri wa miaka 74 alikuwa miongoni mwa wanaume watatu walioshtakiwa katika mahakama ya New York kwa kujaribu kushawishi sera za kigeni wakati Trump anagombea urais mwaka 2016.
Barrack anashtakiwa kwa kula njama, kuzuia haki na kutoa taarifa za uongo kwa maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI Juni 20, mwaka 2019.
Aidha mahakama ya Shirikisho ya Brooklyn pia imemshtaki Matthew Grimes wa Aspen, Colorado na Rashid Sultan RAshid Al malik Alshahhi wa Umoja wa Falme za Kiarabu.