KAMPALA, UGANDA

RAIS Uganda Yoweri Museveni amesema umefika wakati kwa jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa shirikisho la kisiasa, ambalo litawaunganisha zaidi wananchi wa kanda hiyo.

Museveni alieleza hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na naibu rais wa Kenya, William Ruto ambaye alifanya ziara nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya Uganda, Museveni alisema kufikiwa kwa shirikisho la kisiasa kwa nchi za Afrika Mashariki kutawaunganisha zaidi wananchi wa Afrika Mashariki.

“Nimefurahi kusikia baadhi ya wananchi katika kanda yetu hii wanaanza kufikiria uwepo wa shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki na kwmaba shirikisho hilo litaleta nguvu kubwa”, alieleza taarifa hiyo.

Kwa upande wake naibu rais wa Kenya, William Ruto alisema “Tunahitaji pahala wa kuwa na nguvu zitakazotuunganisha kuwa wamoja katika jumuiya yetu”, alisema.

Kwa sasa jumuiya ya Afrika Mashariki kila nchi inaserikali yake inayojitegemea na mifumo tofauti ya kisiasa.