KAMPALA, UGANDA

ABIRIA wanaokwenda Uganda kwa kutumia ndege aina ya Uganda Airlines walichelewa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini, Dar es Salaam nchini Tanzania kwa saa kadhaa baada ya kuishiwa mafuta kwa ndege hiyo.

Kwamujibu wa taarifa zilizotolewa na  gazeti la Daily Monitor ndege hiyo ilieleza sababu ya kuchelewesha safari yake ni kutokana na kuchelewa kupokea mafuta ambayo walikuwa wameyaagiza.

Aidha uongozi wa kampuni hiyo ya ndege iliandika taarifa katika mitandao ya kijamii kuomba radhi kwa tukio lililotokea na kuhaidi tukio hilo kutojirudia siku zijazo.