NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya wanawake ya New Generation Queens ya Zanzibar imepangwa kundi B kwenye michezo ya kufuzu mashindano ya klabu bingwa wanawake Afrika.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu huko nchini Misri, ambapo kila Kanda itaanza Mashindano yao ya Kanda kupata wawakilishi watakaokwenda Misri.
Kwa upande wa kanada ya CECAFA Mashindano hayo yatafanyika Jijini Nairobi nchini Kenya kuanzia Julai 17 hadi Agosti 1, 2021.
Kwa mujibu wa makundi hayo kundi A litakuwa na timu za Lady Doves (Uganda), PVP Buyenzi ( Burundi), Simba Queens-(Tanzania), kndi B Commercial Bank of Ethiopia ( Ethiopia), Uri Joint stars( South Sudan) na New Generation Queens (Zanzibar)
Kundi C lina timu za Scandinavian Fc ( Rwanda),FAD club (Djibout) na Vihiga Queens ( Kenya).
Bingwa wa kila Kanda atafuzu moja kwa moja katika Mashindano hayo makubwa ambapo wenyeji Misri watapewa nafasi moja ya ziada kuingia moja kwa moja kwenye Mashindano hayo, ambayo yatakuwa na jumla ya timu nane kutoka Kanda tofauti ikiwemo ya CECAFA, UNAF, WAFU zone 1, WAFU zone 2, UNIFFAC na COSAFA.