NEW YORK, MAREKANI

GAVANA wa jiji la New York nchini Marekani, Andrew Cuomo ametangaza hali ya tahadhari kufuatia kuongezeka kwa visa vya ufyatuaji risasi katika jimbo hilo.

Gavana huyo amelazimika kuchukua hatua hiyo kufuatia zaidi ya watu 51 kuuawa mwishoni mwa wiki iliyopita katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo kutokana mashambulizi ya bunduki.

Cuomo alisema kumekuwa na ongezeko la vifo vinavyotokana na mashambulio ya bunduki kote nchini Marekani, ambapo vifo 200 vilitokea mwishoni mwa juma pekee katika maeneo mbali mbali ya Marekani.

Agizo gavana huyo, litakwenda sambamba na kutengwa kwa dola milioni 138.7 kwa ajili ya mipango ya kuingilia kati na kuzuia ghasia za bunduki.

Kuanzia mwezi Mechi hadi Mei mwaka 2020, kulikuwa na ongezeko la mashambulizi na uhalifu wa kutumia bunduki katika jimbo la New York na katika maeneo mengi ya Marekani.

Gavana aliamua kuchukua uamuzi wa kuongeza usalama katika maeneo yenye hatari ya kiusalama, pamoja na kutoa mafunzo ya kazi kwa watu wanaoishi katika maeneo masikini.

IMwezi Machi mwaka huu shirika la ujasusi la Marekani (FBI) lilitoa ripoti ya awali ya takwimu za mwaka 2020 zilizoonesha kupanda kwa asilimia 25 ya mauaji yanayotokana na mashambulizi ya silaha ikilinganishwa na mwaka uliopita 2019.