ZASPOTI

MIAMBA ya Misri ya Al Ahly wameitandika Kaizer Chiefs magoli 3-0 nchini Morocco na kuwa klabu ya kwanza katika historia kutawazwa mabingwa wa Afrika mara 10.

Pambano hilo lilipigwa kwenye dimba la Stade Mohamed VI jijini Casablanca.
Mshambuliaji aliyekuwa kwenye kiwango bora, Mohamed Sherif aliifungia Ahly goli la kuongoza baada ya kuwekewa pasi safi, akitumia faida kamili baada ya Happy Mashiane wa Kaizer kufukuzwa nje ya uwanja muda mfupi kabla ya mapumziko.

Mashiane alitolewa nje baada ya kumkanyaga beki wa kulia wa Ahly, Akram Tawfik, akimuacha mwamuzi, Pacifique Ndabihawenimana bila ya chaguo jengine ila kumtoa nje baada ya ukaguzi wa ‘VAR’, hapo awali alikuwa amemuonesha kadi ya njano tu.

Ahly ilifaidika haraka katika kipindi cha pili, kwanza kupitia kwa Mohamed ‘Afsha’ Magdy kabla ya Amr El Solia kumaliza mchezo.
Ikiwa na mataji hayo 10 ya Afrika, sasa Ahly inawazidi mara mbili wapinzani wao wa karibu wa jiji la Cairo, Zamalek na TP Mazembe ya DR Congo zikiwa na ubingwa huo mara tano.

Kocha wa Al Ahly, Pitso Mosimane, anasonga mbele kwa kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Wamisri wakitetea kombe hilo walilolitwaa mwaka jana wakati ushindi wake wa kwanza, na mkubwa zaidi, akiwasili akitokea Mamelodi Sundowns mnamo 2016.

Moja ya mafanikio yake ya kawaida, kwani tokea ikiwasili dhidi ya timu aliyoiunga mkono akiwa kijana, ilimfanya kuwa kocha wa pili wa Al Ahly kushinda Afrika miaka miwili mfululizo, baada ya Manuel Jose wa Ureno mnamo 2005 na 2006.

Ahly iliingia kwenye mchezo huo ikiwa nafasi kubwa, na rekodi yao ya kucheza fainali 14 kwenye soka la Afrika ikiwabeba dhidi ya Kaizer inayocheza kwa mara ya kwanza.
Ikicheza chini ya kocha mpya, Stuart Baxter, akichukua kibarua rasmi kwa mara ya kwanza, Chiefs walikuwa kwenye mechi hadi Mashiane alipotolewa kwa kadi nyekundu, akiamua fainali hiyo kuelekea kwa klabu iliyofanikiwa zaidi katika historia ya Afrika.

Kabla ya mchezo huo, Mosimane alikuwa amedokeza kwamba atakata laini ya mashambulizi ya mipira kutoka pembeni na kuwashika Chiefs na kwa hivyo ilidhihirika kwani Waafrika Kusini hao walishindwa kutafuta njia ya kumpita kipa wa Ahly, Mohamed El Shenawy.

Ahly imepanda kwa mataji 22 ya Afrika wakati Chiefs bado ina moja tu, Kombe la Washindi wa Afrika ambalo walilibeba mnamo 2001, lakini, baada ya kumaliza nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu ya Misri, pointi 31 nyuma ya mabingwa Sundowns, kufikia fainali ilikuwa mafanikio yenyewe.

Wakati huo huo, Al Ahly wataendelea kusonga mbele na watatumai kusisimua kwenye Kombe la Dunia la Klabu kwa mtindo sawa na 2020 walipowashinda Palmeiras ya Brazil na kuupeleka mchezo kwa mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali ya kuvutia ya kichapo.

Kabla ya hapo, El Shenawy na wenzake watano wa Ahly wana nafasi zaidi ya kucheza wanapokwenda Tokyo kushiriki soka ya Olimpiki wakiwa na timu ya taifa ya Misri baadaye mwezi huu.

Al Ahly ilianza kutawala soka na kutwaa mataji ya Misri katika miaka ya 1940 na kuanza kupata mafanikio makubwa katika ngazi ya Afrika katika miaka ya 1980 na kuanza kutwaa taji la mabingwa Afrika mwaka 1982 na 1987.
Klabu hiyo iling’ara tena katika michuano ya Afrika katika miaka ya 2001, 2005, 2006, 2008 ikiwa chini ya kocha Mreno Manuel Jose na mwaka 2012, na baadae mwaka 2013.

Miamba hiyo imepata mafanikio zaidi kuliko klabu nyengine yoyote Afrika, ambapo mwaka 2001 ilisherehekea kuvikwa taji la klabu ya karne Afrika na kucheza na Real Madrid ambayo ilishinda goli 1-0.
Mbali na kutwaa mataji, Al Ahly pia ndio klabu iliyofuzu mara nyingi kucheza michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.

Klabu hiyo imekuwa ikidhaminiwa na makampuni tofauti kwa miaka kadhaa zikiwemo Adidas, Puma, Nike, Vodafone na Etisalat ya Misri.(Ahram Online Sports).