RIO DE JANEIRO, Brazil
MATAIFA hasimu kwenye soka, Brazil na Argentina yatakutana kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Copa America 2021 inayofanyika jijini Rio de Jenairo, Brazil.
Itakuwa fainali kati ya Lionel Messi wa timu ya taifa ya Argentina dhidi ya Neymar wa Brazil kwenye uwanja wa Maracana, Julai 11.

Argentina imeshinda hatua ya nusu fainali mbele ya Colombia kwa penalti 3-2 baada ya kipa, Emiliano Martinez kuokoa penalti tatu, baada ya muda wa kawaida kwenye wa uwanja wa Mane Garrincha kumalizika kwa sare 1-1.

Mapema, Brazil ilitangulia fainali ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Peru katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza katika uwanja wa Nilton Santos.
Argentina haijashinda taji hilo tangu ilipofanya hivyo mwaka 1993 wakati Brazil wameshinda Copa America mara tisa huku mara zote tano wakibeba taji hilo wakiwa wenyeji.

Mshindi mara sita wa tuzo ya Ballon d’Or, ambaye anaangalia kushinda kombe lake la kwanza kubwa na Argentina alimwagia sifa mlinda mlango wake, Emiliano Martinez, kwa kuokoa mikwaju mitatu ya penalti.

“Ilikuwa ngumu wakati mwengine,” Messi alisema. “Lakini tuna ‘Emi’ na ni mzuri. Tulimuamini”.Argentina:Emiliano Martinez, Nahuel Molina, German Pezzella, Nicolas Otamendi, Nicolas Tagliafico, Rodrigo De Paul, Max Rodriguez, Giovani Lo Celso, Lionel Messi, Lautaro Martinez na Gonzalez.

Colombia: David Ospina, Oscar Munoz, Yerry Mina, Davinson Sanchez, William Tesillo, Juan Cuadrado, Wilmar Barrios, Anderson Diaz, Rafael Borre, Gustavo Cuellar na Duvan Zapata. (BBC Sports).