LONDON, England
KLABU ya Brentford imekamilisha uhamisho wa mchezaji wa kwanza baada ya kupanda Ligi Kuu England, usajili huo ni wa nyota wa kimataifa wa Nigeria, Frank Onyeka akitokea FC Midtjylland.

Kiungo huyo anajiunga na Brentford kwa kandarasi ya miaka mitano ambapo fedha za usajili zimefanywa siri.Onyeka (23), baada ya kujiunga na timu hiyo, alisema, atajitenga mwenyewe kwa angalau siku 14 kabla ya kujiunga na wenzake mazoezi ambao sasa wanaendelea wakijiandaa na msimu ujao 2021/22.”Tunafikiria atakuwa ingizo nzuri kwetu”, alisema, kocha Thomas Frank.

Brentford itacheza EPL msimu ujao kufuatia kuwa nje kwa takribani miaka 74, wakipata nafasi hiyo kufuatia ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Swansea City katika mchezo wa mtoano.Onyeka mpaka sasa amecheza mechi moja pekee ngazi ya kimataifa akiwa na Nigeria ingawa anaweza akateuliwa kwenye Afcon ya mwaka 2022.(BBC Sports).