NA TUWERA JUMA ‘MCC’
NAIBU Katibu Mkuu Mufti wa Zanzibar, Fahim Hafidh Hassan amewataka waumini wa dini ya kiislamu kujitokeza kwa wingi kusajili madrasa na miskiti iliyopo katika shehia zao.
Aliyasema hayo huko ofisini kwake Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili alisema watu watakapo jitokeza itawaondoshea usumbufu pale wanapotaka kutoa elimu.
Alisema kufanya hivyo itawapa wepesi pale panapotokezea misaada mbali mbai kutoka sehemu tofauti, kwani itakuwa rahisi wa kuzitambua zinapo patikana na kuwa na takwimu sahihi .
Alifahamisha kuwa usajili unasaidia kupata haki zako zote kutoka serikalini ,ukitaka kufunguwa benki akauti itakulazimu uwe na usajili, pamoja na kuomba misaada kutoka nje .
Alisema jumla ya miskiti iliyopo Unguja ambayo tayari imeshasajiliwa ni 1,775 , na madrasa za Unguja 1,893 na kwa upande miskiti 2,870 na madrasa 4,947 .
Alisema wanampago maalum wakuanzisha hapo badae wa kuweka misikiti na madrasa kama mfumo wa skuli na walimu watakuwa wale ambao waliopatiwa mafunzo maalumu yanayotolewa katika ufisini kwao.
“Wito wangu kwa waumini wazangu wa dini ya kislamu wajitokeze kwa wingi kuja kuzisajili madrasa na misikiti ambayo ipo katika shehia zao ili waunge mkono juhudi za serikali ya awamu ya nane “alisema Fahim.