BUDAPEST, HUNGARY

WAZIRI mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema kuwa juhudi za Umoja wa Ulaya za kuilazimisha nchi hiyo kuifutilia mbali sheria mpya inayopiga marufuku kukuzwa kwa vitendo vya ushoga skuli hazitofaulu.

Orban amesema serikali yake haitoruhusu wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja skuli.

Kiongozi huyo wa siasa za mrengo wa kulia ameyasema hayo katika siku ambayo sheria hiyo mpya imeanza kutekelezwa ya kupiga marufuku skuli kutumia nyenzo zinazoonekana kama zinashajihisha ushoga na vitendo vya kubadili jinsia, na kusema watu walio chini ya umri wa miaka 18 hawawezi kuonyeshwa picha zenye maudhui ya ngono.

Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa UIaya Ursula von der Leyen ameionya Hungary ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya kuwa lazima iibatilishe sheria hiyo au ikabiliwe na nguvu kamili za sheria za Umoja wa Ulaya.