NA MADINA ISSA
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema ni vyema uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA) ikazingatia maslahi na thamani ya walimu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa lengo la kukuza ubora elimu na maendeleo ya sekta hiyo.
Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msngi katika ujenzi wa madarasa katika skuli ya Mtoni Kidatu, alisema endapo kukiwa na mazingira bora kwa walimu itapelekea kutolewa elimu iliyokuwa na kiwango.
Alisema, kazi ya ualimu ni heshima katika nchi hivyo, wizara ione umuhimu wa kuendelea heshima hiyo kwa kuwaboreshea maslahi yao pamoja na misahara yao ili ufanisi uweze kupatikana zaidi.
Pamoja na hayo, alipongeza kamati ya wazee wa watoto wanaosoma katika skuli hiyo pamoja na wadau wengine wa elimu kwa juhudi zao walizozichukua ikiwemo viongozi wa jimbo hilo, katika kuhakisha ujenzi huo unafanikiwa na kuwataka kuendelea kushirikiana na serikali kuongeza nguvu ya kuimarisha miundomnibu mbali mbali ya hduma za jamii.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kuja huku Kidatu, nimeona kwa macho yangu changamoto ya barabara nitalichukua kwakushirikiana na wenzangu tutahakikisha tatiz hili linandoka mara moja,” alisema.
Hata hivyo, aliwataka wazazi na walezi kuendelea kuwapa moyo watoto wao na kuasaidia masomo yao Kwani ulimwengu uliopo wa sasa ni elimu kwanza.
Akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Simai Mohammed Said, alisema serikali kupitia wizara ya elimu itahakikisha inaungaisha nguvu ili kuona elimu inakuwa Zanzibar kwa kasi kikubwa.
Alisema hivi sasa wizara hiyo inaendelea kutafuta fursa mbali mbali katika kuhakikisha changamoto inayoikabili sekta ya Elimu inakuwa historia nchini na wanafunzi wanasoma katika mazingira bora.
Aidha aliwataka wazazi na walezi wa skuli hiyo, kushirikiana na walimu katikakuwasimamia watoto wao ili kuona ufaulu unaengezeka katika skuli na wanafunzi kufanya vizri katika mitihani yao ya taifa.