PARIS, Ufaransa
KOCHA Mkuu, Mauricio Pochettino, amesaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja na Paris St-Germain ambao utamuweka klabuni hapohadi mwaka 2023.
Bosi huyo wa zamani wa Tottenham awali alisaini mkataba hadi mwaka 2022 wakati bosi huyo mwenye umri wa miaka 49 alipochukua jukumu mnamo Januari.

Pochettino, ambaye alikuwa nahodha wa PSG kama mchezaji kutoka 2001 hadi 2003, alikuwa akihusishwa na kurejea Spurs kabla ya uteuzi wa Nuno Espirito Santo.

“Nina furaha, kwangu mwenyewe na pia kwa wafanyakazi wangu”, alisema, Pochettino.
“Ni muhimu kwetu kuhisi imani ya klabu na tutatoa kiwango chetu cha juu ili mashabiki wajivunie Paris St-Germain.
“Ndiyo sababu tutajaribu kufikia malengo yetu kwa pamoja, kama kitu kimoja. Miaka ishirini iliyopita nilikuwa nahodha wa klabu hii na leo mimi ndiye kocha. Ni ndoto iliyotimia”.

Msimu uliopita Pochettino aliiongoza PSG kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo ilitolewa na Manchester City, na walichapwa na Lille kushinda taji la ‘Ligue 1’.
Lakini, Mwenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ana imani Pochettino ndiye mtu sahihi kuiongoza klabu hiyo kupata mafanikio zaidi.(BBC Sports).