JAKARTA, INDONESIA

RAIA zaidi wa kigeni wamekuwa wakiondoka nchini Indonesia kufuatia ongezeko la idadi ya visa vya virusi vya korona nchini humo, linalosababishwa na kuenea kwa kasi kwa aina mpya ya virusi ya Delta iliyogundulika mara ya kwanza nchini India.

Indonesia ilithibitisha visa vya korona 30,000 hadi 50,000 kwa siku mwezi huu.

Iliripoti vifo 2,069 wiki hii, hiyo ikiwa idadi kubwa zaidi ulimwenguni kwa siku moja.

Maofisa wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Soekarno-Hatta karibu na mji mkuu wa Jakarta wanasema raia wa kigeni chini ya 20,000 waliondoka nchini humo kila mwezi kuanzia mwezi Januari hadi Mei.

Walisema idadi hiyo ilizidi 20,000 mwezi uliopita, na hadi sasa kumekuwa na raia wa kigeni 20,215 walioondoka nchini humo mwezi huu.