NA MWAJUMA JUMA

RAIS wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) Abdullatif Ali Yassin, amesema bado yumo katika mchakato wa kuangalia mtu sahihi ambae ataweza kumteua kuwa Makamu wa Rais wa shirikisho hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema hadi sasa hajajua nani atamteua kushika wadhifa huo na kuwa msaidizi wake katika utekelezaji wa majukumu ya kuliendeleza soka la Zanzibar.

Alieleza hivi sasa anaandaa utaratibu wa kumpata Katibu Mku wa shirikisho hilo na baadae kuunda kamati na mara baada ya kumalizika hayo atakuwa tayari amempata makamu wake.

“Nipo katika mchakato wa kuangalia ni nani hasa nimteue kushika wadhifa huu, lakini kwa sasa akili yangu inanituma mpaka nitakapokuwa na Katibu Mkuu na kuunda kamati zangu hapo mambo yatakuwa sawa,” alisema.