NA TUWERA JUMA (MCC)

MKUU  wa Mkoa wa Mjini Magharibi,  Idrisa Kitwana Mustafa, amewaomba wanachi katika shehia ya Mboriborini na Mwanyanya kwa Gowa, kuwa na imani na viongozi wao, ili kuendelea kuwatatulia changamoto zao .

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachi wa shehia hizo  katika  ziara yake yakusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuweza kuzifanyia kazi.

Alisema kufanya hivyo ni kufuata amri na utaratibu uliowekwa na Raisi kwa kuwataka wakuu wote kutembelea sehemu mbali mbali za miji , vijiji na vitongoji kwa lengo la kusikiliza changamoto zao .

Alifahamisha kuwa pesa zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtoni wanakusudia kuzinunulia vifaa mbali mbali vitavyokabidhiwa kwa vijana wanaojishughulisha na kuweka mazingira safi, ili wasivunjike moyo, na kuwaletea watalamu wa kuja kuwapatia elimu  juu ya uhifadhi wa taka hizo.

Alisema baadhi ya changamoto zinazowakabili  wanachi ni vyema viongozi kuzichukuwa kwa ajili ya kuzifanyia kazi ili kuzitatuwa kwa haraka.

“Nawaomba wananchi wasikate tamaa kwani viongozi wao tupo kwa ajili yao kuweza kuwatatulia vikwazo vyao “, alisema kitwana.