MADRID, Hispania

KLABU ya Real Madrid imegoma kumuongezea mkataba beki wao Raphael Varane ambaye anatajwa kuwaniwa na Manchester United.

Nyota huyo awali ilikuwa inaelezwa kuwa mabosi wa Real Madrid hawakuwa tayari kumuuza kwenda Manchester United kutokana na mpango wao wa kumpata Paul Pogba kugonga mwamba.

Kwa sasa inaelezwa kuwa Varane yupo kwenye mazungumzo na Manchester United nayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskajer ambaye anahitaji saini ya beki huyo.

Ikiwa Varane ataondoka ndani Madrid itakuwa ni pigo jingine kwa timu hiyo kwa kuwa iliachana na beki wao kisiki, Sergio Ramos ambaye mkataba wake ulimalizika na hakuongeza mwingine.