PARIS, UFARANSA
KARIBU mataifa 200 yameanza majadiliano kwa njia ya mtandao ya mabadiliko ya tabia nchi, yenye lengo la kuipa nguvu ripoti ya kisayansi ya Umoja wa Mataifa ambayo itaongoza mjadala huo wenye lengo la kuunusuru ulimwengu na majanga.
Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa duniani, Patteri Taalas aliwaambia kiasi ya wajumbe 700 kupitia mtandao wa Zoom, kwamba ripoti hiyo ambayo wanakwenda kuihitimisha itakuwa muhimu kwa dunia.
Alisema tathmini ya jopo la wajumbe wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yanayojulikana kama IPCC itakuwa muhimu kwa mafaniko ya mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabia nchi wa Glasgow, ambao utafanyika Novemba 1 hadi 12.