TURIN, Italia
KLABU ya Juventus ipo tayari kumuachia nyota wao, Cristiano Ronaldo kujiunga na Paris Saint- Germain ili kupata saini ya Mauro Icardi.

Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri, ameweka wazi anahitaji huduma ya Icardi kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao na mabosi wa Juventus wanapambana kuinasa saini yake.

Lakini nayo PSG wakiweka wazi kuwa wanamuhitaji Ronaldo.Mfungaji huyo bora wa michuano ya Euro 2020 hivi karibuni aliweka wazi kuwa hataki kubakia Juventus, licha ya kwamba mpaka sasa amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja.

Nyota huyo iwao atahamia PSG ataungana na Mbrazili, Neymar Junior.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 anaonekana kukosa furaha na ‘Bibi Kizee’ hicho cha Turin baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Italia msimu huu.(Goal).