KIGALI, RWANDA

WIZARA ya Afya nchini Rwanda imesema iko tayari kuanzisha uchunguzi juu ya Hospitali binafsi ya Kimataifa ya Baho, katika kituo chake kilichoko Kigali, baada ya wagonjwa kadhaa kutumia mitandao ya kijamii kulalamika juu ya uwendeshaji wa hospitali hiyo.

Uchunguzi huo ulitangazwa na Daktari Daniel Ngamije, wa wakati akijibu ujumbe wa Twitter zilizokuwa zikitumwa na watu kadhaa ambao walikuwa wakipinga ubora wa huduma ambazo hospitali hiyo inatoa.

Inaelezwa mtumiaji wa mitandao ya kijamii hakutoa maelezo mengi juu ya uzoefu wake, lakini malalamiko mengine yalifuata kutoka kwa watumiaji wengine ambao walidai kuwa na uzoefu mbaya na hospitali hiyo ya Nyarutarama.

Akizungumza na The New Times, Ofisa Mahusiano ya Umma wa Hospitali ya Kimataifa ya Baho Janvier Munyaneza alisema malalamiko hayo yamewashangaza kwani hakuna mteja aliyewahi kuwaendea hapo awali, akilalamikia.

“Tuna nambari za simu na timu ya utunzaji wa wateja ambayo inapokea malalamiko na maoni, lakini hatujawahi kupokea malalamiko juu ya huda tunazozitoa. Kwa hivyo, hatuna taarifa juu malalamiko hayo,”alisema.

“Tunatoa usafi kwa sababu hospitali inapaswa kuwa na safi kila mara, hivyo tunapata wateja wengi, haswa wa kimataifa, na hakuna njia ambayo unaweza kuwapokea bila viwango bora vya usafi. Kwetu, kiwango chetu cha usafi kiko juu,” alisema kwa msisitizo.

Aidha kuhusu hatua ya wizara kutaka kufanya uchunguzi juu ya suala zima la huduma zinazotolewa na hospital hiyo, Munyaneza alisema kuwa hana shaka yoyote na watampa ushirikiano mzuri.