MINSK, BELARUS

MAAFISA nchini Belarus wameifunga tovuti ya chombo maarufu cha habari za mtandaoni, na kikawakamata waandishi wake kadhaa na kufanya upekuzi unaoyahusisha mashirika matatu ya habari.

Inaelezwa kuwa matukio hivi karibuni kumekuwa na ukandamizaji mkubwa dhidi ya wapinzani na vyombo huru vya habari katika taifa hilo lililokuwa sehemu ya muungano wa Kisovieti.

Wizara ya habari ya Belarus imesema imeifunga tovuti ya shirika la Nasha Niva vaada na ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu kulituhumu kwa kuchapisha habari zisizo halali ambazo hazikuelezwa.

Chama cha Waandishi wa Habari cha Belarus – BAJ kimesema maafisa walipekua ofisi za Nasha Niva na kumkamata mhariri mkuu Yahor Martsinovich na mhariri Andrey Skurko.

Aidha maafisa hao wa ujasusi walipekua ofisi za vyombo vya habari vya kikanda, Brest Gazette mjini Brest kwenye mpaka na Poland na Inter-press katika mji wa Baranovichi.