NA MWANDISHI WETU , RUKWA

CHAMA cha Mapinduzi  kimesema hakitaacha kutetea maslahi ya umma, kupigania maendeleo ya kisekta au kutofuatilia ahadi zilozotolewa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kwani masuala hayo yameahidiwa na hayana budi kutekelezwa kwa muda muafaka .

Kadhalika chama hicho tawala kimeapa kufuatilia utelelezaji wa kazi zote zilizoahidiwa na chama na mtendaji yeyote atakayezembea kizembe atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Msimamo huo, umetolewa jana na katibu wa NEC itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka, kwa nyakati tofauti na wazee, wenyeviti wa mashina na viongozi wa Chama hicho wilaya ya Sumbawanga vijijini akiwa katika ziara ya Siku mbili akiambatana na Katibu Mkuu, Daniel Chingolo.

Alisema kazi ya CCM tokea enzi za TANU na ASP ni kushughulika na maisha ya watu, shida na kero zao lakini pia kutazama kwa kina iwapo mikakati ya kimaendeleo iliobuniwa kisera katika maeneo husika ili yanaatekelezwa hatimaye utelelezaji huo utoe matokeo chanya.

Amefahamisha kuwa Chama hicho  ndicho chenye dhamana ya kuzisimamia serikali zote mbili na endapo mambo yatazingwa na urasimu chama kitachukua hatua kwa kufuata taratibu husika.