NA MWANDISHI WETU

BAADA ya kuwa na asilimia kubwa ya kutetea ubingwa wa ligi kuu Bara kwa mara ya nne mfululizo, Kocha Mkuu Didier Gomes, amesema atawapumzisha baadhi ya wachezaji waliotumika sana na kuwapa nafasi wengine.

Gomes amewataja nyota hao Miraji Athuman, Said Ndemla, Gadiel Michael na David Kameta kuwa wanafanya vizuri mazoezini, na anafurahi kufanya nao kazi lakini kutokana na ukubwa wa kikosi wameshindwa kupata nafasi.

Gomes alisema msimu ulikuwa mrefu na wachezaji walipambana na kufanikisha kunatetea ubingwa, hivyo kwenye mechi tatu za ligi zilizosalia atawapa nafasi nyota wengine ambao hawajacheza mara nyingi.

“Tunashukuru tumefanikiwa kutetea ubingwa wetu, nadhani tutawapumzisha wachezaji waliocheza mechi nyingi na kuwapa nafasi wengine sababu msimu ulikuwa mrefu.