NA TIMA SALEHEDAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Simba SC umesema akili yao yote ilikuwa  kutwaa ubingwa wa ligi Kuu Tanzania Bara na sasa wanaelekeza nguvu kwenye kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Simba hivi karibuni  wametangaza ubingwa kwa mara ya nne mfululizo kwa kuwachapa Coastal Union mabao 2-0

Baada ya mchezo huo Simba watakuwa wamebakisha michezo miwili ambapo mmoja utachezwa  kesho Alhamisi dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi.

Mchezo huo ulitakiwa kuchezwa Julai 14 ila ratiba ilibadilika  kutokana na ajali iliyotokea Julai 9 iliyowahusisha baadhi ya wachezaji wa kikosi  cha  Polisi Tanzania

Wekundu hao wa msimbazi watacheza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Namungo nakukabidhiwa kombe lao ligi kuu.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana Ofisa habari msaidizi wa klabu ya Simba Ali Shatri alisema wametawazwa mabingwa na wanajiandaa kwenda kuchukua ubingwa  Kigoma.

Alisema kwa sasa hawajaanza kufikiria kimataifa kwanza wanamaliza kazi yao iliyoko mbele yao.