NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imeridhia matakwa ya msemaji wa klabu hiyo Hajji Manara kutoendelea kuhudumu nafasi ya msemaji wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Hajji Manara, aliandika barua ya kutaka kuachia nafasi hiyo na imekubaliwa.
Manara amefikia hatua hiyo baada ya kuvuja kwa sauti ambazo zilisikika akimlalamikia Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez, kuwa anamfanyia hujuma za kutoka aonekane anaihujumu timu hiyo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Barbara alisema amesikia maneno hayo yanayosambaa, lakini kwa wakati huo alikuwa hawezi kujibu kwa kuwa alikuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu, Simba imemteua Ezekiel Kamwaga, kukaimu nafasi hiyo ya mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ya klabu kwa muda wa miezi miwili.
Kamwaga anauzoefu wa kutosha kwenye tasnia ya habari kwani amewahi kufanya kazi na klabu ya Simba, pia alifanya kazi ndani na nje kama mwanahabari kwa zaidi ya miaka 15.
Alisema uongozi unamshuku Hajji kwa huduma yake aliyoitoa kwenye klabu kwa moyo wake kwa kipindi chote alichokuwepo.