NAIROBI, KENYA
WALIMU nchini Kenya wameelezea wasiwasi wao juu ya msongamano wa wanafunzi katika skuli na nafasi duni wakati Covid-19 inaendelea.
Utafiti uliotolewa na Tume ya huduma ya Walimu unaonyesha skuli zina wasiwasi juu ya kutolipa ada kwa wazazi walioathiriwa na Covid-19.
Utafiti huo unaonyesha asilimia 30 ya walimu walikuwa na wasiwasi jinsi Covid-19 itakavyosimamiwa katika skuli zilizojaa watu wengi kwani nchi inatarajia wimbi la nne la ugonjwa huo.
Utafiti huo ulifanywa wakati wa likizo iliyomalizika tu na ulihusisha walimu 5,176.
Skuli za msingi na sekondari zilifunguliwa kwa kalenda ya skuli ya 2021.
Pamoja na kubadilika kwa kalenda ya skuli ya sekondari, asilimia 23 ya walimu walioshiriki katika utafiti huo walisema wanaharakia kumaliza mtaala kutokana na vizuizi vikubwa vinavyowakabili.
Kulingana na utafiti huo, asilimia 13 ya walimu waliohojiwa walitabiri kuongezeka kwa kazi.
Skuli za Sekondari pia zitatarajia kuongezeka kwa idadi ya watu na wanafunzi wanaoingia wa Kidato cha kwanza watakaodahiliwa Agosti .
Mwaka huu, idadi iliyodahiliwa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza itafikia rikodi ya wanafunzi milioni 1.17.
Asilimia kumi na sita ya walimu walisema msongamano na miundombinu duni na nafasi ni jambo kuu ambalo linaweza kusababisha matatizo.
Mtendaji mkuu wa TSC Nancy Macharia alielezea kiwango cha utayari wa walimu katika usimamizi wa Covid-19 na unahitaji kuimarishwa.