NA IDARA HABARI MAELEZO
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema kuibuka kwa vitendo vya ukusanyaji wa fedha kutoka kwa wananchi kwa kutumia jina la uwekezaji unaoendelea katika maeneo mbali mbali nchini haupo chini ya usimamizi wa Serikali.
Taarifa iliyolewa na Idara ya Habari Maelezo, imeeleza kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, ukusanyaji huo hufanyika ama kwa njia ya fedha taslim au kupitia mitandao.
Taarifa hiyo imewataka wananchi wa Zanzibar kuwa, shughuli hizo ambazo hufanywa na vikundi vya watu pamoja na baadhi ya Kampuni ikiwemo Kampuni ya PAMA FUNDS, Qnet, GAMEAS, WOZUR na nyenginezo sio salama.
Hivyo, Serikali imeeleza inatoa tahadhari kwa wananchi kwamba, ni vyema kujiepusha na ushiriki wa biashara hizo, ili kuepusha upotevu wa mali zao.