NA MWAJUMA JUMA

CHAMA cha Soka la  Ufukweni kimetoa kalenda yake kwa ajili ya msimu wa 2021/2022.Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho  Ali Sharif Adolf, katika hafla ya fainali za michuano ya ZIFF Women Beach Soccer iliyomalizika hivi karibuni.

Alisema kalenda hiyo ilikuwa izinduliwe wakati wa fainali hiyo, imeonesha masuala yote ya kimichezo, ambayo yatafanywa na chama hicho ndani ya msimu huo.

Hivyo alisema mbali ya kuwa haikuzinduliwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, lakini tayari msimu mpya umeanza kupitia mashindano hayo.

Alieleza kwamba licha ya mashindano hayo kuingia katika tamasha lakini kalenda yao inaonesha  msimu wao umeanza  vyema.

“Tumeanza kufungua kalenda yetu kupitia mashindano haya kalenda hii ilikuwa  izinduliwe na kumkabidhi rais wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu amekosekana”, alisema.