GALGUDUUD, SOMALIA

JESHI la Somalia limetangaza kuwa limekomboa kitongoji Al -Shabaab katika jimbo la Galguduud kutoka kwenye makucha ya kundi la kigaidi la Ash-Shabaab.

Msemaji wa serikali ya Somalia, Mohamed Ibrahim Moalimuu ameeleza katika taarifa kwamba vikosi vya usalama katika eneo la Damugh, vikishirikiana na vikosi vya jeshi.

Vikosi hivyo vilifanya operesheni ya shambulio na kufanikiwa kukikomboa kitongoji cha Ammarah baada ya mapigano makali na kundi la kigaidi la Al -Shabaab.

Wanamgambo wa kundi hilo walilazimika kukimbia katika mapigano hayo. Taarifa zinasema, wapiganaji wa pande zote mbili walijeruhiwa katika makabiliano hayo.

Ammarah ni kitongoji cha pili kukombolewa na jeshi la Somalia tangu mwanzoni mwa wiki hii.

Moalimuu aliongeza kuwa, hivi sasa askari wa jeshi la nchi hiyo wanasonga mbele kwa lengo la kukikomboa kitongoji kingine cha Sijru kinachodhibitiwa na Al –Shabaab.

Mwishoni mwa wiki iliyopita askari wa jeshi na wanamgambo katika kitongoji cha Baadwin walitangaza kukombolewa kitongoji hicho kilichoko kwenye eneo la Madj kutoka kwenye makucha ya kundi hilo la kigaidi.