NA MARYAM HASSAN

Waziri Afisi ya Raisi Kazi Uchumi na Uwekezaji,  Mudrik Ramadhani Soraga, amesema Zanzibar bado inanafasi nyingi za kuwekeza katika kukuza uchumi wake  na tayari  serikali imeweka mipango madhubuti katika suala zima la uwekezaji.

Akizungumza na  ujumbe wa watu wanne wa kampuni ya Kalipsca kutoka Maputo Msumbiji  ambayo inashughulika  na masuala ya uvuvi alisema   kuja kwa ujumbe huo kunaleta matumaini katika utekelezaji wa kukuza  sekta ya uchumi wa bluu nchini.

Alisema Zanzibar inaeneo kubwa la bahari ikiwemo visiwa vidogo vidogo hivyo uwekezaji katika suala la uvuvi ni hatua nzuri ya kuwepo usarifu wa mazao ya baharini.

Aidha Waziri Soraga alisema kuwa, amefurahishwa  na ujumbe  huo kwa kuja kuwekeza Zanzibar kwani hatua hiyo itachangia kuendeleza shughuli za kuimarisha ukuaji uchumi.

Hata hivyo,  aliwashauri wawekezaji hao kukutana na uongozi wa uchumi wa bluu na  mamlaka ya vitega uchupi (ZIPA) kwa kupata maelekezo zaidi ili waanze utekelezaji wa kazi zao.