JUBA, SUDAN KUSINI
NCHI ya Sudan Kusini imekuwa ikikabiliwa na njaa tangu nchi hiyo ijipatia uhuru wake miaka 10 sasa, inaelezwa kuwa wakaazi bado wanakabiliwa na tatizo la usalama wa chakula licha ya kuwepo ardhi kubwa na yenye rutba.
Mwezi uliopita ripoti kutoka shirika la chakula ulimwenguni, WFP, limeonya kuwa asilimia 60 ya wakazi milioni 7.2 wa Sudan Kusini wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula kwenye robo ya kwanza ya mwaka huu.
Kulingana na mwenyekiti wa taasisi ya kiuchumi ya Sudan Kusini, Laku Likang, taifa hilo linaagiza asilimia 80 ya chakula kutoka mataifa ya nje, vyakula kama mboga na tungule huku vyengine vikiagizwa huagizwa kutoka Ugand
Akizungumza katika kipindi cha VOA cha South Sudan in Focus, Lukang amesema kwamba tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake, bado halijaweza kubuni viwanda vya kutengeneza bidhaa kama vile mafuta ya kupikia au sukari.
Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya taifa hilo kuwa na mafuta ghafi, fedha zinazopatikana zinahitajika kununua vifaa muhimu vya kilimo kama matrekta ili kuongeza uzalishaji wa chakula.