JUBA, SUDAN KUSINI

KATIKA muda wa siku chache zijazo, nchi ya Sudan Kusini itakabiliwa na uhaba wa chanjo za kukabiliana na ugonjwa wa corona.

Hivi karibuni wizara ya afya nchini humo ilieleza kuwa imeingiza chanjo 72,000 za AstraZeneca, hata hivyo kutokana na utoaji wa chanjo unaoendeleza kutolewa umesababisha upungufu mkubwa.

Kwa mujibu wa ofisa wa kukabiliana na ugonjwa wa corona nchini humo, Angelo Guop, alisema wizara hiyo kwa sasa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa corona ambapo imebakiwa na chanjo zisizozidi 1,820.

“Idadi ya chanjo zilizobakia haizidi 1,820 ambazo zipo katika hospitali kubwa ikiwe ni pamoja na hospitali kuu iliyopo mjini Juba, hospitali ya kijeshi na hospitali ya jeshi la polisi”, alisema.

Alifahamisha kuwa hadi kufikia Julai 18 kuna uwezekano kuwa chanjo hiyo itakuwa imemalizika na nchi hiyo haitakuwa na chanjo ya corona.