KABUL,  AFGHANISTAN

KUNDI la Taliban limependekeza kusitisha mapigano kwa muda wa miezi mitatu kwa masharti kuwa serikali itawaachia huru wafungwa 7,000.

Aidha mjumbe mmoja kati ya wajumbe wa serikali wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya amani na Wataliban, Nader Nadery, ameongeza kuwa waasi hao pia wamedai kuondolewa kwa viongozi wao kwenye orodha ya majina ya wakosowaji ya Umoja wa Mataifa.

Haikubainika mara moja ni kwa namna gani serikali itajibu pendekezo hilo la kusitisha mapigano, ambalo limetolewa wakati ambapo Marekani inaongeza kasi ya kuviondoa vikosi vyake, katika mchakato unaotazamiwa kukamilika Agosti 31.

Hata hivyo vikosi vya usalama vya Pakistan vimetumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya watu waliojaribu kuingia nchini humo kwa nguvu, kutoka Chaman hadi mpaka wa Spin Boldak nchini Afghanistan.

Inaelezwa kuwa mpaka huo ulifungwa na mafisa wa Pakistan baada ya Taliban kuiteka Spin Boldak na kupandisha bendera zao mjini humo.