LONDON, England
BEKI wa pembeni wa Manchester United, Alex Telles, atakosa mechi za mwanzoni mwa msimu ujao kufuatia maumivu ya kifundo cha nguu ambayo aliyapata kwenye mazoezi wiki iliyopita.
Telles (28), anaweza kukosa mechi za mwanzoni dhidi ya Leeds United, Southampton na Wolves.
Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema, walitegemea angelirudi uwanjani mapema, lakini, mambo yamekuwa tofauti na atakaa nje kwa muda sasa.
Telles ni chaguo la pili United baada ya Luke Shaw ambapo alicheza mechi 23 msimu uliopita.(Goal).