LONDON, England

POLISI wa Metropolitan nchini England wamethibitisha kuwashikilia watu tisa ambao wamehusika na vurugu baada ya mechi ya robo fainali ya EURO 2020 kati ya England na Ukraine.

Tukio limetokea baada ya mechi, wakati Polisi wakidhibiti uwepo wa mikusanyiko mikubwa ya watu jijini London ambao walikuwa wakishangilia England kuingia nusu fainali.

Kati yao, watatu wanatuhumiwa kuwajeruhi askari wawili. Katika mchezo huo England ilishinda 4-0.