LONDON, England
KLABU ya Everton imemsajili winga wa zamani wa England, Andros Townsend na kipa mzoefu, Asmir Begovic.
Townsend (30), alijiunga kwa uhamisho wa bure kufuatia kumalizika kwa mkataba wake huko Crystal Palace na amesaini mkataba wa miaka miwili na ‘The Toffees’.
Begovic (34), amesainiwa kutoka Bournemouth kwa kandarasi ya miezi 12 na chaguo la mwaka zaidi.
“Kila kitu kiko mahali kwetu kwa mafanikio”, alisema, Begovic ambaye atatoa msaada kwa Jordan Pickford.Kuwasili kwa Townsend huko Goodison Park kunamshuhudia akiungana tena na meneja mpya wa Everton, Rafael Benitez, ambaye alifanya naye kazi Newcastle United.
“Everton ni klabu kikubwa,” aliiambia, EvertonTV. “Nataka kudhibitisha kuwa ninatosha kuwa mchezaji muhimu hapa.”Townsend, aliyecheza mechi 13 za kimataifa za nchi yake, alianza soka yake katika akademia ya Tottenham Hotspurs, akitumia miaka saba White Hart Lane kabla ya kuhamia Newcastle mnamo Januari 2016. (BBC Sports).