TUNIS, TUNISIA
WAZIRI wa Mambo ya nje wa Tunisia amewapigia simu wenzake wa Uturuki, Ufaransa, Italia, Ujerumani, Umoja wa Ulaya na Kamishna wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa baada ya hatua ya rais wa taifa hilo kusimamisha shughuli za bunge na kuivunja serikali ya taifa hilo.
Taarifa ya wizara hiyo, iliyotolewa ilisema hatua zilizochukuliwa na Serikali ya taifa hilo zilikuwa za muda mfupi na kwamba wenzake waliahidi kuiunga mkono demokrasia changa ya taifa hilo.
Hatua ya hivi karibuni iliyoshangaza wengi ya Rais Kais Saeid ya kumfukuza waziri mkuu na mawaziri wengine kadhaa na kulisimamisha bunge kwa siku 30 ililiingiza tena taifa hilo katika vurugu za kisiasa.